Timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) imetinga fainali ya kombe la CECAFA Senior Challenge baada ya kuwaondoa mabingwa watetezi Uganda kwenye mchzo wa nusu fainali uliomalizika jioni hii.
 
Mchezo huo umepigwa kwenye uwanja wa Moi mjini Kisumu, ambapo Zanzibar walifanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 22 kupitia kwa Abdulaziz Makame Hassan kabla ya Uganda kusawazisha dakika ya 28 kupitia kwa Nsibambi Derrick.
 
Aidha, kipindi cha pili Zanzibar ilianza kwa kasi huku wakitumia mbinu za mashambulizi ya kushitukiza ambapo katika dakika ya 58 walifanikiwa kupata penati ambayo ilifungwa na mchezaji, Mohamed Issa Juma. ambapo bao hilo limeipeleka Zanzibar fainali.
 
Kwa ushindi huo wa vijana hao wa kocha Hemed Morocco, watakutana na timu mwenyeji ambayo ni Harambee Stars waliofuzu hatua ya fainali baada ya kuwafunga Burundi bao 1-0.
 
  • Ratiba mpya ligi kuu Tanzania bara
  • Mwansasu atangaza kikosi cha taifa soka la ufukweni
  • Ujio wa timu ya Olimpiq Stars ya Burundi
 
Hata hivyo, Kenya na Zanzibar zote zimetoka kundi A ambapo Kenya iliongoza kundi hilo ikifuatiwa na Zanzibar Heroes iliyoshika nafasi ya pili.

Singida Utd yamsajili Papaa Kambale, vijana 4 wa Serengeti boys, Danny Lyanga
Ujio wa timu ya Olimpiq Stars ya Burundi