Idadi ya wagonjwa wa kisukari nchini imebainika kuongezeka kwa kasi kutoka 1% hadi 9% kwa watu wenye umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, kutokana na aina ya vyakula na mtindo wa maisha ya wananchi.

Hayo yamebainishwa jana na Profesa Andrew Swai ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Kisukari, katika mjadala kuhusu ugonjwa huo jijini Dar es Salaam uliohudhuriwa na madaktari bingwa.

Profesa Swai alieleza kuwa ongezeko hilo la ugonjwa wa kisukari unatokana na tabia za wananchi wengi kula vyakula visivyokuwa na virutubisho vya kutosha.

“Hii inatokana na wananchi wengi kula ugali wa unga uliokobolewa (sembe) badala ya kula dona, kunywa matunda yaliyokamuliwa kupitia juice badala ya kula matunda yenyewe pamoja na mambo mengine,” alisema Profesa Swai.

“Bia pia inaongeza sana uwezekeno wa kupata kisukari. Kwa sababu ukinywa bia unaongeza uzito, na ukianza kuona unanenepa na kuongezeka uzito sana ujue kuna tatizo,” aliongeza.

Profesa Swai alisema kuwa pamoja na vyakula hivyo visivyo na virutubisho, wananchi wengi wanaugua presha/kisukari kutokana na kutofanya mazoezi.

Lowassa adai anawaumiza CCM, awafungukia wanaotaka kufukuzwa kwa ajili yake
Picha: Ne-Yo na Mkewe wapata baraka ya mtoto