Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema Wizara hiyo inatekeleza miradi ya maji ya kimkakati katika mkoa wa Shinyanga inayogharimu shilingi bilioni 35 ambayo itasaidia wananchi wa mkoa huo kuondokana na changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama.

Aweso ameyasema hayo mjini Shinyanga, wakati wa uwekwaji wa Jiwe la Msingi Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria utakaohudumia eneo la Tinde na Shelui ukitarajia kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 24.4.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

Amesema, pamoja na wananchi wa kata ya Tinde kunufaika na mradi huo pia vijiji 22 vya Jirani vitaweza kufikiwa na mradi utakaowasaidia wananchi kupata maji safi na salama.

Aidha, ameongeza kuwa Wizara hiyo itaendelea kufuatilia na kusimamia utekelezwaji wa miradi ya maji, ili ikamilike kwa wakati na kutoka huduma kwa wananchi na kufanikisha azma ya kufikisha maji kwa asilimia 95 maeneo ya mijini, na asilimia 85 maeneo ya vijijini ifikapo mwaka 2025.

Bumbuli aibukia Simba SC, amtetea Mgunda
Rais avunja Bunge na kuitisha uchaguzi