Mkurugenzi wa ufundi wa Gwambina FC Mwinyi Zahera ametoa ufafanuzi kuhusu kuitwa kwenye timu ya taifa ya DR Congo kwa kiungo wa Young Africans Tonombe Mukoko.

Tonombe alitajwa kwenye orodha ya wachezaji wa DR Congo watakaounda kikosi kitakachokabiliwa na michezo ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa Barani Afrika (AFCON 2022), dhidi ya Gabon na Angola itakayochezwa baadae mwezi huu.

Zahera ambaye ni sehemu benchi la ufundi la timu ya taifa ya DR Congo, amefafanua suala hilo kufuatia sintofahamu ilioibuka kwa baadhi ya wadau wa soka nchini, ambao wameonesha kuwa na wasiwasi juu ya kuitwa kwa kiungo huyo, aliesajiliwa na Young Africans mwanzoni mwa msimu huu akitokea AS Vita Club.

“Tonombe Mukoko yupo ndani ya kikosi cha kwanza cha timu ya Taifa ya DR Congo cha wachezaji 45 ambao wameorodheshwa mwezi mmoja kabla ya michezo,”

“Alitumiwa barua ya kujulishwa kwamba yupo kwenye orodha ya wachezaji wanaoweza kuitwa kwenye kikosi, lakini pia inawezekana asiitwe.”

“Ijumaa hii tutaita wachezaji rasmi, zamani tulikua tunaita wachezaji 23 wa mwisho, lakini Kutokana na Covid-19, tutataja wachezaji 33.”

“Hivyo Tonombe Mukoko ameorodheshwa katika majina yale 45, lakini bado hajaitwa katika orodha ya mwisho, inawezekana aitwe au asiitwe.” Amesema Mwinyi Zahera ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha Young Africans.

Ufafanuzi huo umelazimika kutolewa na Mwinyi Zahera kufuatia Uongozi wa Young Africans kumpongeza Mukoko Tonombe kupitia kurasa za mitandao ya kijamii, baada ya kuwa sehem ya wachezaji waliotajwa kwenye kikosi cha DR Congo.

Kim Poulsen: Sivunji benchi la ufundi Stars
31 waitwa The Cranes