Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, kupitia ripoti zake mbili za matukio ya utatanishi kuanzia mwaka 2020-2022, imesema machafuko yanayoendelea katika nchi ya Jamhuri ya Afrika ya kati (CAR), yanaweza kuwa uhalifu wa kivita

Kamishna Mkuu wa Haki zabinadamu wa Umoja wa Mataifa, Michelle Bacehelt akiwa 

 Geneva Uswisi amesema, taarifa hiyo imetolewa kufuatia uchunguzi uliofanywa na kitengo cha Haki za binadamu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuimarisha utulivu nchini CAR- MINUSCA

Ripoti ya kwanza, inahusu tukio lililotokea kati ya tarehe 6 mpaka 13 Desemba, 2021 ambapo wanamgambo walishambulia kijiji cha Boyo kilichoko mkoa wa Ouaka na kuwaua watu 20, kubaka wasichana, kuchoma, kupora na kusababisha zaidi ya wanakijiji 1000 kuyakimbia makazi yao.

Ripoti hiyo imesema, ”wanamgambo walioshambulia raia kwa mapanga, walishikilia mamia ya raia kwa siku tatu ndani msikiti wa kijiji wakiwatishia kuwaua wakidaiwa kuunga mkono kikundi cha UPC kinachopingana na serikali.”

“Ninalaani vikali vitendo hivi, Serikali lazima ikomeshe ukiukwaji huu, iwe unafanywa na vikosi vyake, wanamgambo au wanajeshi wote wachukuliwe hatua na iwawajibishe moja kwa moja,” amesema Kamishna Mkuu Bacehelt.

Aidha, ripoti hiyo pia imethibitisha mienendo ambayo imekuwa ikirekodiwa na MINUSCA ya wakandarasi wa kijeshi wa kigeni, wanaofanya kazi chini ya maelekezo au kwa idhini ya serikali ambapo wanakuwa wakitumia washirika wao kuendeleza mashambulizi dhidi ya raia.

Naye Mkurugenzi wa kitengo wa haki za binadamu wa MINUSCA, Hana Talbi amesema, “kwa vile washirika hawa ni wapiganaji wa zamani kutoka kwenye makundi mbalimbali yenye silaha au wapinga Balaka, matokeo ya kuishi pamoja kwa amani yanaleta wasiwasi.”

Rais Samia alia ajali Mtwara
Kiungo wa Ismailia aishawishi Simba SC Misri