Idara ya Uhamiaji imetangaza rasmi uzinduzi wa huduma ya fomu ya maombi ya pasipoti mtandaoni (Online Passport Application Form), huduma hiyo kuanza rasmi siku ya Jumatatu ya tarehe 7 Agosti, 2017.

Na inapenda kuwatangazia Umma kuwa huduma hiyo itapatikana kupitia tovuti yao ya https://www.immigration.go.tz/ppt_application/.

Kufuatia uzinduzi wa huduma hiyo, imeawaomba waombaji wote wa pasipoti kujaza fomu hizo mtandaoni kisha kuzichapisha  na kuziwakilisha katika ofisi za uhamiaji.

Hata hivyo, matumizi ya huduma hii yataenda sambamba na huduma inayotumiwa sasa ya fomu za maombi ya pasipoti mpaka pale itakapotangazwa vinginevyo.

Utaratibu wa namna ya kujaza fomu hizo umeelekezwa katika fomu husika mtandaoni, na pia wateja wanaweza kupata ufafanuzi.

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma waombaji wameshauriwa kutembelea anuani ya Idara ambayo ni  info@immigration.go.tz au katika Ofisi yoyote ya Uhamiaji iliyo karibu nao.

 

Bomba la mafuta kuleta ajira 10,000 vijiji 184
Mkuu wa Wilaya awasweka ndani wajumbe wa bodi ya Mkula