Msemaji Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanda ametoa taarifa rasmi kuhusu kusitishwa kwa matumizi ya pasipoti ya zamani zinazosomeka kwa mashine hadi ifikiapo Januari 31, 2020.

Akitoa taarifa hiyo kwa umma pia amewataka watu wote wanaotarajia kusafiri safari za nje ya nchi hivi karibuni kuhakikisha wanabadilisha pasipoti zao hadi kufikia julai mwaka huu ili kuondokana na usumbufu utakaojitokeza uwanja wa ndege na sehemu za mipakani wakati wa safari zao.

Ameongezea kuwa kisheria pasipoti inatakiwa kuwa hai angalau miezi 6 ili iweze kuombewa visa ya nchi anayokwenda na kuruhusiwa kuondoka.

Hatua hiyo ni kufuatia kuzinduliwa na kuanza kutumika kwa pasipoti mpya za kielektroniki.

Aidha, Mtanda amesema ujenzi wa miundombinu wa kuwezesha utoaji wa pasipoti hizo za kielektroniki tayari umekamilika katika mikoa na ofisi za balozi za Tanzania 23 zilizopo nje ya nchi.

Akizitaja kwa majina ni pamoja na Uingereza, Ufaransa, Marekani, New York, Israel , Saudi Arabia, Comoro, Italia, Nigeria, Nairobi, Ujerumani, Algeria, Misri, Uholanzi, Ubelgiji, Zambia, India, Malawi, China, Malaysia na Uholanzi.

Hivyo idara ya uhamiaji inawakumbusha watanzania wote waliopo ndani na nje ya Tanzania kuwa matumizi ya pasipoti ya zamani rasmi yatasitishwa ifikapo Januari 31, 2019.

 

Video: Jinsi Makonda, Mambosasa walivyomtia mbaroni mmiliki wa kitambulisho feki kariakoo
Cassper Nyovest akatishwa tamaa na muziki wa Afrika Kusini