Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa baadhi ya Wakuu wa Mikoa ambapo sasa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imesema, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatma Abubakar Mwassa amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, huku Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert John Chalamila akihamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imesema uhamisho huo wa Wakuu wa Mikoa umeanza mara moja.

Chalamila aacha wosia Karagwe, akina mama watabasamu
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Mei 16, 2023