Kikao cha mawaziri wa sheria wa kundi la nchi tajiri kiviwanda la G7 kimesema mashambulizi ya makombora yanayofanywa na Urusi dhidi ya miundo mbinu ya nishati nchini Ukraine, ni uhalifu wa kivita kisheria .

Hayo yamebainishwa na Kiongozi wa kikao hicho ambaye ni Waziri wa sheria wa Ujerumani, Marco Buschmann na kuongeza kuwa, kampeni ya Urusi ya mashambulizi ya makombora yameiharibu vibaya miundo mbinu ya nishati, nchini Ukraine.

Moja ya mashambulizi yanayotajwa kuleta uharibifi nchini Ukraine. Picha ya The Telegraph.

Amesema, hatua hiyo imesababisha mamilioni ya watu kuwa katika kiza wakati nchi hiyo ikijiandaa kushuhudia theluji ikianguka kwa mara ya kwanza nchini humo katika msimu huu pamoja uwepo wa baridi na upepo mkali.

Mkutano huo wa G7 pia ulihudhuriwa na Waziri wa sheria wa Ukrain na mwendesha mashtaka mkuu wa nchi hiyo huku Waziri wa sheria wa Ujerumani, Marco Buschmann akisema ana uhakika watashuhudia kesi za uhalifu wa kivita katika mahakama ya kimataifa ya jinai ICC dhidi ya viongozi wa Urusi.

Singida Big Stars ruhsa kusajili Dirisha Dogo
448 wauawa katika maandamano: IHR