Rais Uhuru Kenyatta amesema hawezi kufanya kazi na kiongozi yeyote ambaye ni tapeli na hutumia nafasi yake kuhadaa Wakenya.

Katika kile kilichoonekana kama mishale ya kisiasa kwa naibu wake William Ruto, Rais Kenyatta alisema kuna kiongozi muongo ambaye hawezi kumuunga mkono.

“Aki ya Mungu mimi mtu wa maongo hatuwezani, haki ya Mungu mimi hatuwezani, na mimi nasema hivyo kwa roho safi,” alisema Rais Uhuru na kuwatahadharisha wakazi dhidi ya kushawishika na siasa za Ruto akisema kuwa ni za kuhadaa wananchi.

Rais Uhuru alisema Ruto alipiga vita mkataba wa mabadiliko ya katiba BBI kiwango cha kuufanya kutofaulu ilhali ulikuwa usaidie raia.

“Mlikuja hapa mkadanganywa eti BBI ni mbaya, na ilikuwa ya kuwafaa Wakenya. Sasa ngojeni mtaona, kwa sababu mliskiza hao,” alisema Uhuru.

Hata hivyo, wandani wa DP Ruto wanakosoa muenendo huo wa Rais Uhuru wakisema amemgeuka kiongozi msaidizi wake huyo wakati huu ambapo hamhitaji.

“Kwani leo ndio Rais Uhuru amejua Ruto ni muongo. Huu ni unafiki na ukora mkubwa sana wa kisiasa ambao lazima tumalize Kenya. Yeye alisaidiwa 2013 na 2017 na Ruto lakini sasa anasema hayo, maliza uende,” Mbunge wa Gatundu Moses Kuria alisema.

Rais Uhuru Kenyatta hata hivyo amesema hana tatizo na Ruto lakini asipewe Urais katika uchaguzi wa mwaka huu ambao umekuwa na joto kali ikiwa na upinzani kati ya upande unaungwa mkono na Rais aliyeko madarakani na upande wa aliyekuwa naibu Raisi.

Mwanahabari azirai hewani
Kesi ya kina Mdee na wenzake kusikilizwa kesho