Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametangaza mpango wenye vipengele 8 kwa ajili ya kuchochea uchumi wenye thamani ya Ksh. Bilioni 53.7 ili kukabiliana na madhara ya Covid 19.

Amesema Serikali imetenga Ksh. 6.5 Bilioni kwa Wizara ya Elimu kuajiri walimu 10,000 na wakufunzi 1,000 wa teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT) ili kusaidia programu ya kujifunza kidijitali.

Aidha amesema kuwa sekta zitakazonufaika ni pamoja na miundombinu, elimu, biashara, kilimo, mazingira, utalii na afya ambapo watumishi wapya 5,000 wataajiriwa, pia Ksh. Bilioni 1.7 imetengwa kwa ajili ya kuongeza vitanda katika hospitali za umma.

Rais Kenyatta amesema Serikali imekuwa ikitoa jumla ya Ksh. 250 Milioni kwa wiki kwa familia zilizokumbwa na hali ngumu ya maisha kutokana na mlipuko wa corona.

Hata hivyo amesema visa vipya 31 vimeongezeka na jumla ya maambukizi imefikia 1,192. Kenya imepima sampuli 57,650 tangu kuanza kwa mlipuko wa virusi vya corona.

Ummy atoa majibu ripoti ya uchunguzi maabara ya corona "mashine ina hitilafu"
Lindi: Madiwani sita wa upinzani wahamia CCM