Wasanii wa muziki nchini wanaofanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee na Juma Jux ambao wapo katika mahusiano ya kimapenzi wameamua kuandaa ziara inayojulikana kama In love & Money Tour yenye lengo la kuhamasisha muziki mzuri na kujiweka karibu na mashabiki wao ili waweze kujua maisha yao halisi na ya kimuziki.

Vanessa Mdee amesema kupitia ziara hiyo watatoa fursa kwa vijana mbalimbali ili kuwawezesha kimaendeleo ambapo ametaja kwa kuanza wameandaa shoo yao katika mikoa minne ya kitanzania ambapo watafanya shoo itakayoonesha maisha yao halisi na jinsi ambavyo wanafanya kazi.

”In love and Money tour ni maisha yetu sisi, sisi tupo kwenye mahusiano lakini tunafanya kazi ya muziki kwahiyo tunajaribu kama maisha yetu kuyaweka katika ukweli fulani na mashabiki wetu waone” amesema Jux.

Ameongezea kuwa wanatumia pesa nyingi katika muziki wanaoufanya, lakini wanajikuta hawafanyi shoo yeyote kutokana na malipo ya chini yanayopatikana katika shoo ambazo wanaitwa kuzifanya.

Hivyo wameamua kujitolea kuanzisha matamasha yao wenyewe wakitegemea ushirikiano mkubwa kutoka kwa mashabiki zao na wasanii wengine

”Imefikia hatua wasanii wanaukubwa ambao wanaweza wakiamua kujitegemea na kuandaa shoo zao kubwa nadhani hata duniani pia matour mengi yanafanyika na wasanii wakubwa na sio tena kupigiwa simu kufanya shoo watu wanaandaa shoo zao” Jux.

Aidha Jux amesema kwa Tanzania wao ni wasanii wa kwanza kufanya kitu kama hiko kwa wasanii kuandaa show zao wenyewe.

 

Sakata la matibabu ya Wabunge lamuibua Msekwa

Comments

comments