Chama cha Conservative kinachoongozwa na Boris Johnson, kimeshinda zaidi ya viti 326 na kujinyakulia ushindi katika uchaguzi mkuu nchini Uingereza.

Chama hicho kilihitaji kujipatia viti 326 ili kutangazwa kuwa mshindi lakini hadi sasa kimepitisha idadi hiyo na kufikia viti 334.

Akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi baada ya chama chake kushinda zaidi ya viti 326, Boris Jonhson amesema kwamba hatua hiyo inaipatia serikali mpya fursa ya kuheshimu maamuzi ya kidemokrasia ya raia wa Uingereza ili kuliimarisha taifa hilo.

”Zaidi ya yote nataka kuwashukuru watu wa taifa hili kwa kujitokeza kupiga kura ya Disemba ambayo imebadilika na kuwa ya kihistoria, ambayo inatupatia sisi kama serikali mpya fursa ya kuheshimu uamuzi wa kidemokarsia wa raia wa kulibadilisha taifa hili na kuonesha uwezo wa raia wa taifa hili”. Amesema Jonson.

Hatua hiyo inajiri muda mchache baada ya mpinzani mkuu wa Boris, Jeremy Corbyn kusalimu amri na kusema kwamba hatokiongoza tena chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.

Waziri huyo mkuu amesema kwamba uamuzi huo unampatia jukumu la kufanikisha Brexit na kuiondoa Uingereza katika muungano wa Ulaya.

Huu ni uchaguzi wa Uingereza wa tatu chini ya miaka mitano na wa kwanza kufanyika mezi Disemba katika kipindi cha miaka 100 na umetawaliwa na kura ya maoni ya 2016 ya kuondoka katika muungano wa Ulaya.

Njaa, vilio vya watoto vilimlazimu kusaga Mihogo iliyoua Watoto
Video: Magufuli aonya CCM kuanguka, kanisa lenye masharti ya ajabu nchini