Uingereza imetangaza kifo cha mgonjwa wa Covid 19 alfajiri ya leo mwenye umri wa (13) mvulana ambaye ndiye mdogo zaidi nchini humo kufariki dunia na ugonjwa wa Corona.

Mvulana huyo ambaye familia yake imesema hakuwa akisumbuliwa na magonjwa  mengine amefariki dunia ikiwa ni siku kadha mara baada ya kugundulika na dalili za awali za ugonjwa huo

Kwa mujibu wa The Sun News mapema mwenzi ulipita Ubeligiji iliripoti kifo cha binti wa miaka 12 ambaye alifariki kutokana na ugonjwa Covid 19 hivyo kumfanya binti huyo kuwa mdogo zaidi ndani ya bara la ulaya na pengine duniani kote kufariki kutokana na Covid-19 tangu kuzuka kwa ugonjwa huo.

Hata hivyo hapo awali ilikuwa inaaminika kuwa watoto hawezei kudhurika na ugojwa huo kutokana na mfumo wa kinga zao za mwili kuwa imara zaidi ya watu wengine lakini kifo hiki kimezua maswali mengi miongoni mwa wataalamu nchini humo na duniani kote.

 

Minziro azigonganisha Alliance FC, Pamba FC
Meddie Kagere afichua usioyajua

Comments

comments