Maandamano ambayo yanendelea nchini Uingereza katika bandari ya Bristol, waandamanaji wamevunja sanamu ya karne ya 17 ya mfanyabiashara wa utumwa Edward Colston, hata hivyo maandamano hayo pia yalishuhudiwa mjini Brussels, London, Cologne, Bonn, na Stuttgart.

Wakati huo huo miji ya New York na Chicago nchini Marekani imeondoa amri ya kutotembea nje, kufuatia maandamano ya mwishoni mwa wiki ya kupinga ubaguzi wa rangi na ukatili unaofanywa na polisi mara baada ya kifo cha Mmarekani mweusi Gorge Floyd.

Maandamano hayo ya amani yaliendelea jana mjini New York huku maelfu ya waandamanaji wakifurika katika mtaa wa Manhattan.

Ujumbe wa mtoto wa Floyd “Baba yangu amebadilisha dunia”

Hata hivyo maelfu ya watu walimiminika katika miji mbalimbali ya UIaya kuonyesha mshikamano wao kwa vuguvugu la kupinga ubaguzi dhidi ya watu weusi kufuatia kifo cha Floyd.

Mtandao kusaidia maonesho ya sabasaba 2020

Floyd, aliuawa akiwa amefungwa pingu wakati polisi mzungu wa mjini Minneapolis, alipogandamiza goti lake katika shingo yake kwa takribani dakika tisa hata baada ya kusema kuwa hawezi kupumua.

Wakenya kutotembea usiku kwa siku 30, vita dhidi ya Corona

Mbivu, Mbichi za Man City kufahamika juma hili
Mpina atangaza kibano waingizaji haramu wa maziwa