Uingereza, Ujerumani na Italia zimegundua aina mpya virusi vya corona aina ya Omicron hapo jana huku waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson akitangaza hatua mpya za kukabiliana na virusi hivyo wakati mataifa zaidi yakiweka vikwazo vya usafiri kutoka kusini mwa Afrika.

Waziri wa afya wa Uingereza Sajid Javid, amesema visa viwili vya aina hiyo mpya ya virusi vilivyogunduliwa nchini humo, vinahusishwa na safari za Kusini mwa Afrika.

Wizara ya afya katika jimbo la Bavaria la Ujerumani pia ilitangaza kesi mbili zilizothibitishwa za aina hiyo mpya ya kirusi.

Watu wawili waliingia nchini Ujerumani mnamo Novemba 24 kupitia uwanja wa ndege wa Munich kabla ya Ujerumani kuiorodhesha Afrika Kusini kama eneo hatari la virusi hivyo.

Nchini Italia, taasisi ya kitaifa ya afya imesema kisa kimoja cha kirusi cha Omicron kimegunduliwa mjini Milan kutoka kwa mtu aliyetoka Msumbiji.

Waziri Mkuu autetea utawala wa Taliban
Zahanati hii itapunguza vifo kwa wamama wajawazito- Balozi Ibuge