Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson ameweka kando tishio la kujitoa Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano kuwa kipaumbele cha chama chake cha kihafidhina.

Kwa mujibu wa gazeti la Times, sasa waziri mkuu huyo atazingatia zaidi kuhakikisha kuwa makubaliano mapya aliyoyafikia na umoja wa Ulaya juu ya mpango wa Brexit yanapitishwa.

Awali, Johnson aliahidi kuitoa Uingereza katika umoja wa Ulaya kwa makubaliano au hata bila ya makubaliano Oktoba 31 mwa mwezi uliopita.

Hata hivyo wabunge walipiga kura ya kumlazimisha kutafuta kuongezewa muda zaidi kwa mchakato huo hadi Januari 31 mwaka ujao.

Wanajeshi 35 wauawa kwenye shambulio Mali
Aliyekuwa kocha Yanga apata 'shavu' Zambia