Timu ya taifa ya Uingereza imeshindwa kufurukuta mbele ya timu ya taifa ya Ufaransa kwa kukubali kipigo cha mabao 3-2 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa nchini Ufaransa kwenye dimba la State de France.

Uingereza ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 9 kupitia kapteni wa timu hiyo Harry Kane lakini Ufaransa walisawazisha bao hilo kupitia Samuel Umtiti dakika ya 12.

Djibril Sidibe aliifungia Ufaransa bao la pili dakika ya 43 na mda mchache badae Harry Kane akapachika bao la kusawazisha kwa njia ya mkwaju wa penati dakika ya 48,baada ya Raphael Varane kumchezea vibaya Dele Alli.

Wakicheza pungufu baada ya mlinzi Raphael Varane kuonyeshwa kadi nyekundu timu ya Ufaransa walionyesha kiwango kizuri na kujiamini kwa wachezaji wake mahili na mnamo dakika ya 78 Ousmane Dembele aliipatia Ufaransa bao la tatu na mchezo huo kumalizika kwa Uingereza kupigwa mabao 3-2.

 

🔴Live: Jeshi la Polisi Dar es salaam lapokea magari ya doria
🔴Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Juni 14, 2017

Comments

comments