Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ameahidi taifa hilo kuingia kwenye mchakato wa kusaka nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia 2030.

Kiongozi huyo ametoa ahadi hiyo, baada ya kuridhishwa na maandalizi yaliyofanywa na nchi ya Urusi ambayo ilikua mwenyeji wa fainali za mwaka huu.

Theresa May amesema Urusi wamefanisha kwa kiwango kikubwa maandalizi ya fainali hizo, jambo ambalo anaamini Uingereza wanweza, tena kwa kiwango cha hali juu zaidi.

Kwa upande mwingine amewataka viongozi wa chama cha soka FA, wasisite kuwasilsiha maombi muda utakapofika, huku akiwapa uhakika wa kupata ushirikiano wa dhati kutoka serikali kuu ya nchi hiyo.

‘Tumeoena kwa wenzetu Urusi wameweza kwa kiwango kikubwa kuandaa fainali za kombe la dunia na wamefanikiwa, ninaamini na sisi tunaweza, viongozi wa FA msisite kuwasilisha maombi muda utakapofika, tutawapa ushirikiano kwa hali yoyote ile.’ Amesema kiongozi huyo.

England imewahi kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia mwaka 1966, na mwaka huo huo walikua mabingwa wa fainali hizo.

Taifa hilo pia limewahi kuwa mwenyeji wa michuano ya soka ya bara la Ulaya mwaka 1996 (Euro 96).

Video: IGP Sirro aje ofisini aniambie, Jeshi la Polisi limenyoosha mikono kwa Majambazi?- Lugola
Video: Jafo ataja kiini Jangwani kushika mkia matokeo kidato cha sita 2018