Rais wa Marekani, Donald Trump amekosolewa vikali kwa kutishia kushambulia maeneo ya hifadhi za tamaduni za Iran.

Trump alitoa vitisho hivyo kufuatia jeshi la Marekani kumuua Kamanda wa Iran, Qasem Soleimani.

Rais huyo wa Marekani alisema kuwa katika maeneo 52 yanayolengwa kushambuliwa na Marekani endapo Iran itajaribu kulipa kisasi ni pamoja na maneo ya hifadhi za kitamaduni.

Hata hivyo, Umoja wa Mataifa na Marekani ni kati ya waliopinga vikali tishio hilo kwakuwa kwa mujibu wa mikataba ya Umoja wa Mataifa uliosainiwa na Marekani pamoja na Iran, maeneo ya kiutamaduni yanapaswa kulindwa.

Mkataba huo uliosainiwa unaeleza kuwa wanapaswa kulinda maeneo ya hifadhi za utamaduni ikiwa ni pamoja na wakati wa vita na migogoro.

Kamanda wa Iran, Qasem Soleimani aliuawa kupitia shambulio la Marekani lililofanywa na ndege isiyo na rubani, Ijumaa iliyopita jijini Baghdad. Shambulio hilo lilitokana na amri iliyotolewa na Rais Trump.

Tukio hilo la mauaji ya Kamanda wa Iran limeongeza taharuki zaidi katika eneo hilo, huku Iran ikiahidi kuwa italipa kisasi na imejitoa rasmi kwenye makubaliano ya mpango wa nyuklia iliyoingia kati yake na Marekani mwaka 2015.

 

Mchungaji amuua mkewe wakati wa ibada, naye ajichinja
Yaliyojiri katika mazishi ya mama Erick Kabendera