Kwa mara ya kwanza Uingereza itakosa waamuzi katika fainali za kombe la dunia, baada ya shirikisho la soka duniani FIFA, kuweka hadharani orodha ya waamuzi watakaochezesha fainali za mwaka huu nchini Urusi.

England imekua ikipeleka waamuzi katika fainali za kombe la dunia mara zote isipokua mwaka 1938.

FIFA wameteua waamuzi 36 watakaochezesha fainali za mwaka huu kutoka mataifa mbalimbali na nchi ambazo zimekosa nafasi hiyo ni England, Scotland, Wales na Ireland ya Kaskazini.

Mwamuzi Mark Clattenburg alikua muingereza pekee katika michuano ya fainali za mataifa ya Ulaya mwaka 2016, hali ambayo ilianza kuonyesha hatari ya taifa hilo kukosa muwakilishi upande wa waamuzi siku za usoni.

Clattenburg, ambaye alichezesha mchezo wa fainali ya michuano hiyo kati ya Ureno na Ufaransa, alitangaza kustaafu Februari 2017.

Hali hiyo iliufanya uongozi wa chama cha soka nchini England kuliomba shirikisho la soka duniani FIFA kupewa nafasi nyingine ya kuwa na mwamuzi kwenye michuano inayosimamiwa na shirikisho hilo, lakini ombi hilo lilikataliwa.

Tayari Uingereza ilikua imeshaandaa orodha ya waamuzi ambao wangewania nafasi ya kwenda katika fainali za 2018 ambao ni Martin Atkinson, Stuart Attwell, Robert Madley, Michael Oliver, Craig Pawson, Anthony Taylor na Paul Tierney.

Howard Webb aliiwakilisha Uingereza katika fainali za kombe la dunia mara mbili mfululizo mwaka 2010 (Afrika kusini) na 2014 (Brazil). Alichezesha mchezo wa hatua ya fainali mwaka 2010 kati ya Hispania na Uholanzi.

Katika hatua nyingine Uingereza pia imekosa nafasi ya waamuzi 63 watakaoendesha teknologia ya Video (VAR) ambao watateuliwa siku chache kabla ya kuanza fainali za kombe la dunia nchini Urusi.

VAR itatumika kwa mara ya kwanza katika fainali hizo, baada ya kuonyesha ufanisi mkubwa wakati wa mmichuano ya kombe la mabara mwaka 2017, iliyofanyika Urusi.

Orodha ya waamuzi walioteuliwa kwa ajili ya fainali za kombe la dunia 2018.

Fahad Al Mirdasi (Saudi Arabia) Alireza Faghani (Iran) Ravshan Irmatov (Uzbekistan) Mohammed Abdulla Mohamed (United Arab Emirates) Ryuji Sato (Japan) Nawaf Abdulla Shukralla (Bahrain) Mehdi Abid Charef (Algeria) Malang Diedhiou (Senegal) Bakary Papa Gassama (Gambia) Ghead Grisha (Egypt) Janny Sikazwe (Zambia) Bamlak Tessema Weyesa (Ethiopia) na Joel Aguilar (El Salvador).

Mark W Geiger (U.S.) Jair Marrufo (U.S.) Ricardo Montero (Costa Rica) John Pitti (Panama) Cesar Arturo Ramos Palazuelos (Mexico) Julio Bascunan (Chile) Enrique Caceres (Paraguay) Andres Cunha (Uruguay) Nestor Pitana (Argentina) Sandro Ricci (Brazil) Wilmar Roldan (Colombia) Matthew Conger (New Zealand) Norbert Hauata (Tahiti) Felix Brych (Germany) na Cuneyt Cakir (Turkey).

Wengine ni Sergey Karasev (Russia) Bjorn Kuipers (Netherlands) Szymon Marciniak (Poland) Antonio Miguel Mateu Lahoz (Spain) Milorad Mazic (Serbia) Gianluca Rocchi (Italy) Damir Skomina (Slovenia) na Clement Turpin (France)

Stand Utd yatangulia nusu fainali ASFC
Liverpool, Man Utd kukutana Marekani