Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameshuhudia utiajia saini wa makubaliano ya awali ya ujenzi wa kiwanda cha saruji ambacho uwekezaji wake ni wa thamani ya Dola Milioni 200.

Hafla hiyo imefanyika mbele ya wajumbe wa Baraza la Ushauri Mkoa wa Dodoma jijini Dodoma, huku Senyamule akiwahakikishia wawekezaji hao mazingira rafiki ya kutekeleza shughuli zao na kuwakaribisha kuwekeza zaidi katika ujenzi wa viwanda vingine.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akishuhudia utiaji saini wa makubalino ya awali ya ujenzi wa kiwanda cha saruji kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani milioni moja kwa mwaka katika Wilaya ya Kongwa.

Amesema, “nawakaribisha Dodoma, Makao Makuu ya Nchi yetu, fursa za uwekezaji ni nyingi wekezeni zaidi katika Mkoa wetu, tunayo ardhi na malighafi ya kutosha.”

Awali, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Dkt Omary Nkullo amesema tayari ekari 500 zimepimwa katika eneo la Pandambili, ambazo ni maalumu kwa ajili ya uwekezaji.

Kwa uopande wake Mwekezaji, Anyid Dmjed Rajab amesema wataendelea kuwekeza katika maeneo mengine katika Mkoa wa Dodoma, kutokana na mazingira rafiki ya uwekezaji na upatikanaji wa malighafi.

Robertinho aitangazia vita Horoya AC Kwa Mkapa
Utunzaji Mazingira: Jafo awapa dozi Wakuu wa Wilaya