Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi, jana imesaini mkataba na serikali ya Japan kuanza ujenzi wa barabara ya juu (flyover) kwenye eneo la Tazara, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya hatua ya kupunguza tatizo la foleni jijini humo.

Ujenzi wa barabara hiyo unaotekelezwa kwa ushirikiano na serikali ya Japan kupitia Shirika La Maendeleo la Japan (JICA), unatarajiwa kuanza mapema mwezi Novemba mwaka huu na kukamilika mwaka 2017 na utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 100.

Akizungumza wakati wa utiaji sahihi wa mkataba huo, waziri wa ujenzi, Dkt. John Magufuli alisema kuwa mradi huo ni muhimu sana kwa kuwa utapunguza tatizo la foleni katika jiji hilo huku akitoa mchanganuo wa gharama za mradi huo.

“Tumekuwa tukizungumza kwamba miradi hii mikubwa kama flyover ambayo cost yake ni bilioni 93, ninaposema bilioni 93 namaanisha gharama ya mkandarasi pamoja na consultant. Lakini serikali pia imeshachangia bilioni 8.6. kwa hiyo mradi wote ni bilioni 100,” alisema.

 

 

 

Raul Atangaza Kustaafu Soka
Updates: Alichokisema J Makamba kuhusu ‘taarifa za chopa ya CCM kuanguka’