Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameagiza machinjio ya kisasa ya Ruvu yaliyotelekezwa kwa muda mrefu kujengwa na kukamillika ifikapo Desemba, 2018.

Ameyasema hayo alipotembelea katika ranchi hiyo, ambapo amesema kuwa ni muhimu machinjio hayo ya kisasa yakamilike ili Tanzania ianze kuuza mazao yatokanayo na mifugo katika masoko ya kimataifa.

Amesema kuwa Tanzania ni nchi ya tatu katika bara la Afrika kwa kuwa na uwingi wa mifugo hivyo hakuna sababu ya kushindwa kuongoza katika  soko la mazao ya mifugo katika masoko ya duniani.

Aidha, amesema kukamilika kwa machinjio hayo kutasaidia kupunguza usumbufu kwa wafanyabiashara wa mifugo ambao wote nawapeleka mifugo yao jijini Dar es Salaam.

Chuo Kikuu Huria kuanza kutoa kozi iliyopigwa marufuku
Marekani yataka mataifa yote kukata uhusiano na Korea Kaskazini