Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah amekutana na ujumbe kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na kufanya mazungumzo ya kukazia ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani, kwenye uhifadhi wa bainuai za Bahari ya Hindi na Maeneo Tengefu ya Ukanda wa Pwani.

Akizungumza mara baada ya kukutana na ujumbe huo katika ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi jijini Dar es Salaam, Dkt. Tamatamah amesema katika Ukanda wa Bahari ya Hindi kutakuwa na miradi mingi ambapo kwa kuanzia Mwezi Agosti Mwaka huu 2022, mradi utafanyika Kaskazini mwa Tanzania katika Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga na Kwale Mkoani Kenya.

Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ishmael Kimirei, Mratibu wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFish) Bw. Nichrous Mlalila na Kaimu Meneja wa Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) Bw. John Komakoma wakiwa kwenye mazungumzo na Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) nchini Tanzania Bw. Ralf Senzel na Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Katrin Bornemann waliofika katika ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilizopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo namna ya kukazia ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani, kupitia mradi wa uhifadhi wa bainuai za Bahari ya Hindi na Maeneo Tengefu ya Ukanda wa Pwani, utakaofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani.

Katibu mkuu huyo mara baada ya kukutana na ujumbe huo ambao ni Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Katrin Bornemann na Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) nchini Tanzania Bw. Ralf Senzel, amesema Tanzania itapata Euro Milioni 2.17 sawa na Shilingi za Kitanzania Bilioni 5.2 kwenye mradi huo katika kipindi cha miaka minne.

Huu mradi una faida unalenga kuhifadhi bainuai, utatoa elimu kwa jamii inayokaa katika maeneo hayo na tunategemea mradi utafanya rasilimali kuwa endelevu kwa muda mrefu na utaongeza kipato kwa wananchi, kwa kuwa wataelimishwa njia mbadala za maisha na kuhifadhi Maeneo Tengefu.” Amesema Dkt. Tamatamah.

Naye Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Katrin Bornemann amesema ana furaha kwamba ushirikiano baina ya Ujerumani na Tanzania katika maeneo ya bainuani na Maeneo Tengefu utakuwa na nguvu katika kuhakikisha Ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi unatunzwa pamoja na kuhakikisha rasilimali zilizopo katika Maeneo Tengefu zinaendelezwa, huku Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) nchini Tanzania Bw. Ralf Senzel, amesema mradi huo utajenga uhusiano mzuri baina ya nchi hizo mbili.

Mazungumzo hayo baina ya Katibu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah na Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Katrin Bornemann pamoja na Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) nchini Tanzania Bw. Ralf Senzel, yamehudhuriwa pia na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ishmael Kimirei, Kaimu Meneja wa Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) Bw. John Komakoma ambapo mradi huo utatekelezwa na Mratibu wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFish) Bw. Nichrous Mlalila. 

Rais Samia aomboleza kifo cha Kiongozi wa UAE
Snoop Doggy atangaza kuinunua Twitter