Siku mbili baada ya kutokea tukio la mauaji yaliyotokana na mtu mmoja kufyatua hovyo risasi mjini Munich, mtu mmoja ameripotiwa kujilipua ndani ya baa na kuejeruhi watu 12.

Serikali ya Ujerumani imeeleza kuwa mtu aliyejilipua ndani ya baa hiyo ni raia wa Syria ambaye mwaka jana alikataliwa kupewa hifadhi nchini Ujerumani.

Mtu huyo alijilipua katika mji wa Ansbach, eneo lililokuwa karibu na tamasha moja kubwa la muziki na kulazimika kuondolewa kwa watu zaidi ya elfu mbili kabla ya tamasha hilo pia kusitishwa.

Ujerumani imekuwa katika hali ya taharuki katika kipindi cha siku za hivi karibuni baada ya Ijumaa watu tisa kuuawa katika shambulizi la ufyatuaji hovyo wa risasi mjini Munich. Siku kadhaa zilizopita, kijana mmoja aliwashambulia watu ndani ya treni kwa kisu na shoka.

Video: 'Rais Magufuli Alikataa Kimemo Changu' - Makamba
JPM Kuongoza Maadhimisho ya Mashujaa Dododma Leo