Msemaji wa Serikali ya Ujerumani, Steffen Seibert amesema kuwa Ujerumani haina mpango wa kupeleka wanajeshi wake nchini Syria kama sehemu ya mchango wake katika kupambana na kundi linalojiita dola la Kiislam.

Vyombo vya habari vya Ujerumani vimeripoti kuwa balozi wa Marekani nchini Syria, James Jeffrey ameitaka serikali ya Ujerumani wiki iliyopita kuchangia askari wa nchi kavu kwenye ushirikiano wa kupambana na IS unaongozwa na Marekani.

Aidha, Seibert amesema kuwa Ujerumani kwa miaka mingi inatambuliwa kwa kiasi kikubwa kimataifa kutokana na mchango wake mkubwa ambao pia unajumuisha mafunzo ya askari wa Iraq, kufanya doria za anga na shughuli za kuziongezea mafuta ndege za kijeshi.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Ujerumani inataka kuendelea na majukumu hayo ambayo hayajumuishi kuwapeleka wanajeshi wake kwenye kikosi cha nchi kavu.

Jeff Bezos na MacKenzie waachana rasmi, Mwanamama achukua utajiri mkubwa
Trump aigeukia Uingereza, ' Sitafanya kazi na balozi wao'

Comments

comments