Wizara ya Sheria ya Ujerumani imeidhinisha ombi la Urusi la msaada wa kisheria katika uchunguzi wa kupewa sumu kiongozi wa upinzani Alexei Navalny, na imewapa jukumu waendesha mashitaka wa serikali kushirikiana na maafisa wa Urusi.

Kupitia ujumbe wa twitter, waendesha mashitaka wa Ujerumani wamesema kuwa ofisi yao imepewa idhini ya kutoa msaada wa kisheria kwa Urusi na maelezo kuhusu hali ya kiafya ya Navalny, kama mwenyewe ataridhia.

Ofisi hiyo imesema haitatoa habari zaidi kuhusu ombi hilo kwa wakati huu huku Urusi ikiwa inaongezewa mbinyo na nchi za Magharibi zikiitaka itoe ufafanuzi kuhusu tukio hilo ambalo inasema haihusiki.

Urusi imesema kuwa itaomba kuwatuma wachunguzi nchini Ujerumani kutafuta ukweli kamili kuhusu kisa hicho cha Navalny, ambaye Ujerumani inasema alipewa sumu ya Novichok inayoathiri mishipa ya fahamu.

Waliotumia jina la Mama Janeth Magufuli wahukumiwa
Harmonize agawa magari kwa wasanii wake