Nyota wa muziki wa bongo fleva Marioo ameitambulisha rasmi kwa mashabiki wake kasha maalum la album yake mpya itakayokwenda kwa jina la ‘The Kid You know’.

Marioo, pia amearifu kuwa amewaandalia mashabiki wake zaidi ya zawadi kwa ajili ya kufurahia uwepo wake na mchango mkubwa ambao amekuwa akipatiwa tangu ameingia rasmi kwenye tasnia ya muziki wa bongo fleva.

Mwanamuziki Marioo.

Hii leo Novemba 25, 2022 ataisimulia hadharani historia fupi ya maisha yake kupitia kwenye moja ya kifurushi cha zawadi aliyoandaa kwa mashabiki wake.

Macho na masikio ya mashabiki wa nyota huyo, yako katika kusubiri kwa hamu kusikia ni aina gani ya mirindimo itakayopatika kwenye album hiyo, ambayo siku rasmi ya kuachiwa kwake bado haijatangazwa.

Simba SC yafanywa Shamba Darasa Kigamboini
Neymar azua hofu kambini Brazil