Shirikisho la soka nchini  (TFF), limetoa kibali kwa Chama cha Soka Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) kusimamia michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa itakayofanyika Uwanja wa Kambarage kwa siku za kesho Jumamosi Desemba 16, 2017 na Desemba 17, mwaka huu.

Michezo hiyo itahusu timu ya Olimpiq Stars ya Burundi ambayo kwa sasa iko Shinyanga kwa ajili ya michezo hiyo ya kirafiki ambako kesho Jumamosi itacheza na Stand United na Jumapili itapambana na Mwadui ya Shinyanga.

Lengo kubwa ya ziara hiyo ni kuzipa timu za mazoezi ili ziweze kufanya vema kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara; pia kupima uwezo wa wachezaji ambao timu hizo za Tanzania zimewasajili katika kipindi cha dirisha dogo na kudumisha ujirani mwema.

SHIREFA imeithibitishia TFF kwamba itafuata itifaki zote kwa mujibu wa taratibu za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Uganda yatepeta kwa Zanzibar Heroes
Mwansasu atangaza kikosi cha taifa soka la ufukweni