Hamisi Mandi, maarufu kama B12 au B Dozen aliyekuwa Clouds FM kwa zaidi ya muongo mmoja na nusu, amekiacha kituo hicho na kuhamia kwa wapinzani wao E-FM.

Mtangazaji huyo aliyekuwa anafanya kipindi cha XXL, amewahi kutajwa kuwa moja kati ya watangazaji bora 10 Afrika, katika miaka ya 2000.

Jana, B12 aliweka kwenye akaunti yake ya Instagram post yenye giza na kuandika ‘BlackoutTuesday’ #BLM. Hiyo ilikuwa ‘hashtag’ tag maarufu jana duniani kote, ikiwa inahamasisha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi. Lakini huenda hii pia inaweza kuwa ilikuwa na maana zaidi ya moja kwa B12. Kiza kilikuwa kinapita kwa muda mbele ya mashabiki wa XXL aliokuwa nao kwa zaidi ya muongo mmoja na nusu.

Hivi karibuni, mtangazaji huyo akiwa kwenye XXL ya Clouds Fm alisikika akisema yuko tayari kusimamishwa kazi lakini alimsifia Diamond Platinumz kwa jinsi alivyo-perform vizuri kwenye Tamasha la ‘African Day Benefit’. Ilikuwa sehemu ya utani. Alimtaja kwa jina la ‘Bwana Almasi’, lakini ilifahamika ni Diamond.

Diamond amekuwa kwenye mgogoro na kituo hicho kwa muda mrefu, na sasa nyimbo zake hazichezwi kwenye kituo hicho.

B12 sasa anaenda kuungana na Jonijoo aliyehama hivi karibuni kutoka Wasafi FM akajiunga na E-FM.

Ushindani katika kiwanda cha vyombo vya habari hasa upande wa burudani inaongezeka. Huku B12 na Jonijoo wakiwa E-FM, Wasafi wao wamemnasa Lil Ommy kutoka Times Fm.

Bei ya mafuta yaporomoka, orodha kamili ya bei kwa kila mkoa iko hapa

20 wakamatwa Katavi kwa ‘kunyofoa’ nyeti za watu

Ripoti: 15 waliuawa na Polisi wakati wa amri ya ‘kubaki majumbani’ kuzuia corona Kenya
Bei ya mafuta yaporomoka, orodha kamili ya bei kwa kila mkoa iko hapa