Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewataka viongozi wa serikali na wale ambao watateuliwa kuwa marais siku zijazo, wahakikishe hawafanyi ubinafishaji wowote wa mashirika badala yake yabaki kuwa chini ya Serikali ili yaendelee kutoa huduma kwa wananchi.

Ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa safari ya Treni ya kuanzia Dar es Salaam, Tanga, Moshi na Arusha ambayo ilikuwa imesimama kufanya shughuli zake kwa takribani miaka 30 ambapo amesisitiza utuzwaji wa miundombinu ya treni hiyo.

” Niwaombe viongozi wenzangu hili liwe fundisho tusikubali tena kubinasfisha vitu vya msingi katika nchi, tulibinasfisha ndege na treni tukaja kuanza upya mimi sitakuwa rais wa maisha lakini natoa ujumbe kwa wale wataokuja baadae hili liwe fundisho hata nchi zilizoendelea mashirika yao hayajabinasfishwa” Amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ametoa msisitizo kwa watanzania kuaminiana ambapo amesema kuwa” Vichwa vya watanzania vina akili mno ninawaomba kupitia mfumo huu wa TRC tuanze kujiamini tutafanya makubwa ambayo wengine hawawezi kuyafanya mabehewa yote ya mizigo 347 yamekarabatiwa hapa, na 20 ya abiria nayo yamekarabatiwa hapa”.

Mahasimu Libya wasaini mkataba wa amani
JPM azindua treni Arusha