Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ ametoa wito kwa Watanzania kuwa na imani na Serikali kuhusiana na utoaji chanjo ya ugonjwa wa corona.

amesema hayo katika hafla ya uzinduzi wa chanjo ya covid–19 iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Lusekelo amesemA ili kupambana na janga hilo lililokumba ulimwengu mzima ni lazima nchi iwe na umoja na kushirikiana kwa pamoja kwani Serikali imejiridhisha vya kutosha juu ya chanjo hiyo.

“Wote tunakubali kwamba corona ni vita na hatuwezi kuishinda kama hatuna umoja, tuna Wizara ya Afya, Waziri Mkuu yupo sidhani kama hawa wenzetu wanaweza kuitoa nchi kafara kwamba watu wapate chanjo halafu wafe, lazima mifumo ya nchi yetu imejiridhisha, haitakuwa 100 kwa 100 kila kitu kina mapungufu lakini tujenge imani,” amesema Lusekelo

“Mimi ni muhubiri wa zamani nilianza kuhubiri injili wakati wa Kambarage niwaombe maaskofu wenzangu tujenge imani kwa Serikali yetu na Wizara ya Afya, tunachanja kwa nia njema kwa ajili ya afya zetu, watakaosema Mzee wa Upako anajipendekeza sawa tu kwani akutukanaye hakuchagulii tusi,” amesema Lusekelo

“Uzuri Tanzania ni nchi ya ajabu katika Bara la Afrika hivyo tusiogope wala kufadhaika kwani tunafanya haya kwa nia njema,”amesema Lusekelo

Kauli ya Hayati Magufuli inapotoshwa - Dkt. Gwajima
Rais Samia akizindua chanjo ya Uviko 19