Mkuu wa upelelezi wa polisi wilaya ya Ukerewe (OCCID) Masoud Mohamed ambaye amefariki dunia ghafla leo, kwa mara ya mwisho aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram jana Alasiri.

Masoud ambaye Siku za karibuni alijizolea umaarufu katika mitandao ya kijamii baada ya video kusambaa ikimuonesha akisoma Quran akiwa kavaa sare za Jeshi aliandika ujumbe juu ya muislamu safi.

“Muislamu safi, ni Yule ambaye watu hawapati madhara kutokana na mdomo wake au mikono yake” Allah atujaalie mwisho mwema tusiwe miongoni mwa watu wabaya !” aliandika Marehemu Masoud.

Hata hivyo wakati taarifa ya kifochake ilipotolewa leo, bado chanzo cha kifo hicho hakijabainishwa.

Wataalamu wa afya kuhudumia wananchi kwa simu saa 24
Waziri Kabudi akabidhiwa dawa ya Corona kutoka Madagascar