Serikali ya Uingereza kupitia vyombo vyake vya habari leo hii, Aprili 24, 2018 imetoa tahadhari kwa raia wanaoishi nchini humo juu ya kuhusika na kufanya maandamano ya kisiasa yanayotarajiwa kufanyika April 26, mwaka huu.

Taarifa hiyo imesema kuna zaidi ya raia 75,000 wanaoingia nchini humo kila mwaka, hivyo imewatahadharisha wananchi wake kujihusisha na maandamano hayo kwa madai kuwa wanaweza kupata madhara kutoka kwa jeshi la polisi.

Tahadhari hiyo imekuja baada ya kudai kuwa maandamano hayo yalishapigwa marufuku hivyo endapo yatafanyika polisi itawalazimu kutumia mabomu ya machozi au silaha za moto kusambaratisha maandamano hayo.

”Hivyo muwe makini sana mnapokuwa kwenye mizunguko yenu muepuke mikusanyiko ya watu wanaoandamana, muda wote muwe mnasikiliza vyombo vya habari, mjue nini kinachoendelea,” imesema taarifa hiyo.

Imeongezea taarifa hiyo kuwa endapo kutakuwa na dharura mawasiliano yafanyike kupitia namba 112 kwa msaada wa haraka.

 

Nyerere ampa ujumbe Rais Magufuli
Jurgen Klopp: Roma hawatacheka na Salah leo

Comments

comments