Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema kuanzia Machi Mosi, 2018 ukaguzi wa magari binafsi utaanza ili kuangalia kama yana vigezo na ubora wa kuwa barabarani na ameongezea kuwa kila gari litalipa stika ya ukaguzi ambayo itauzwa kwa shilingi elfu tatu tu.

Masauni ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani ametoa kauli hiyo leo Februari 23, 2018 wakati akizungumza na wanahabari akitoa tathmini ya mpango mkakati wa awamu ya pili wa kupunguza ajali za barabarani nchini.

Amesema ukaguzi huo utakuwa wa nchi nzima na utafanyika katika vituo vya polisi na maeneo maalimu yatayopangwa.

”Askari yoyote atakayetumia nafasi yake kutoa stika ya gari bila kulifanyia ukaguzi na ilihali halina vigezo vya kupewa stika nataka niwaambie kuwa huu si wakati wake, zama zimebadilika”.amesema Masauni.

Pamoja na hayo Mh. Masauni ameongeza kwamba “Nataka madereva  wa pikipiki ambazo zitakamatwa na kukutwa zimesajiliwa kwa majina ya kampuni badala ya majina binafsi wachukuliwe hatua mara moja”.

Kwa upande wa katibu Mtendaji wa baraza hilo, Fortunatus Musilim amewataka wamiliki wa magari hayo kuyapeleka na kutosubiri kitakachotoea baada ya muda wa ukaguzi kumalizika.

 

Waziri Mwakyembe kuzindua 8 bora ligi ya wanawake
ASFC kuendelea kesho

Comments

comments