Bara la Ulaya linakabiliwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika miongo kadhaa, ambapo karibu asilimia 65 ya E.U. ya eneo ardhi kwa sasa liko chini ya kiwango cha tahadhari ya ukame, kulingana na makadirio.

Mito katika eneo hilo imekuwa ikipungua, kuzorotesha biashara na kusababisha usumbufu kwa kampuni zinazosafirisha bidhaa kama vile mafuta na makaa ya mawe huku ukame huo pia ukifichua mabaki ya meli za Vita vya pili vya Dunia na kutatiza safari za mito za Ulaya.

Kadiri ukame unavyozidi kuongezeka, Uingereza inatazamia kuchakata tena maji taka kuwa maji ya kunywa katika siku zijazo huku Mkuu wa Shirika la Mazingira la Uingereza akisema watu watahitaji kutilia mkazo kuhusu wazo hilo.

Mabadiliko ya hali ya hewa, yanatajwa kuongeza ukame, vimbunga na dhoruba nyingine kubwa ambazo zinatajwa kutukia mara kwa mara na na uwepo wa joto kali kwa maeneo mengi.

Mecky Mexime aitikia wito Taifa Stars
Wataalamu kutathmini athari kinu cha Nyuklia