Uongozi wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid unaendelea kufanya maboresho kwenye Uwanja huo, ili kukamilisha maagizo ya TFF kabla ya mchezo wa pili wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ kati ya Coastal Union dhidi ya Azam FC.

Miamba hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara itakutaka kwenye mchezo huo Jumapili (Mei 29), huku Nusu Fainali ya kwanza ikipangwa kuchezwa jijini Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba kati ya Simba SC dhidi ya Young Africans, Jumamosi (Mei 28).

Mwenyekiti Kamati ya Ukarabati Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Gerard Munisi amesema wanaendelea kufanya maboresho katika Uwanja huo na wapo katika hatua za mwisho.

Amesema kwa sasa wanamalizia ukarabati eneo la vyumba vya kubadilishia, baada ya kukamilisha shughuli za kuboresha eneo la kuchezea ambalo litakua na shughuli pevu siku ya Jumapili (Mei 29).

“Tumeboresha eneo la kuchezea ‘PITCH’ ili kuwa la kisasa, Kwa sasa tunafanya mabadiliko kwenye vyumba vya kubadilishia, tumeboresha ili viendane na mahitaji ya sasa ya mpira wa miguu.”

“Kamati yangu inaamini zoezi hili litakamilika kwa wakati na kila atakaekuja kushuhudia mchezo wa Nusu Fainali kati ya Coastal Union na Azam FC atajionea mabadiliko makubwa yaliyofanywa hapa.”

“Tunaamini Uwanja huu utakuendelea kuwa katika kiwango hiki hata baada ya mchezo wa Nusu Fainali, kwani tumepewa nafasi nyingine ya kuwa wenyeji wa mchezo wa Fainali ya ASFC, utakaochezwa Julai Pili.” amesema Gerard Munisi

CCM Kirumba yazisubiri Simba SC, Young Africans
Barbara Gonzalez, Haji Manara waitwa TFF