Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kukitaka Chama cha Mapinduzi CCM kuboresha viwanja vya michezo vinavyomilikiwa na chama hicho, moja ya tawi la CCM Kata ya Kawe wamepongeza kutolewa kwa kauli hiyo na kusema kuwa hiyo ni hatua kubwa katika uboreshaji wa michezo.

Akizungumza na Dar24Media Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Kawe Potipoti Yusuphu Ndaga amesema ukarabati huo utasaidia upatikanaji wa ajira kwa vijana, lakini pia kwasababu vijana ndiyo nguvu kazi itakuwa ni fursa kwao kutumua viwanja hivyo katika kujiendeleza kimichezo na kupata ajira kupitia kipaji cha mpira.

Amesema CCM itafaidika na mapato kama wamiliki wa viwanja na kukifanya chama kuwa chama ambacho kinajitosheleza kimapato hata bila ruzuku

“Chama cha CCM kitakuwa chama kisichotegemea michango ya wanachama, kitakuwa sio chama kinachopitisha bakuli kwa wadau, kitakuwa chama kimejitosheleza kiuchumi, kupitia viwanja vyake ambavyo mahususi vitaenda kutumika katika michezo ya ligi kuu na ligi mbalimbali na Nchi za jirani,” amesema Katibu Mwenezi Ndaga.

Naye Khassim Ngonyani Katibu Jumuiya ya Umoja wa Vijana CCM, amesema kuwa hali ya mazingira ya viwanja imechangia kushusha maendeleo ya mpira nchini, ambapo kauli ya Rais Samia imeonekani ni hatua kubwa katika kuinua michezo nchini.

Amesema hali ya viwanja ilivyo hivi sasa imekuwa ni changamoto kubwa ametolea mfano Nchi ya Rwanda wanauwezo wa kuendesha michuano mikubwa kutokana na kuwa na viwanja bora, ukilinganisha na viwanja vya Tanzania tunashindwa kuendesha mashindano makubwa.

Ameongeza kuwa endapo ukarabati huo utafanyika kwa wakati utafungua milango ya fursa za kimataifa kwa kuendeleza michezo lakini sio kwa sasa tumejifungia fursa wenyewe.

Sambamba na hayo wamewahasa vijana kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika kulijenga Taifa la Tanzania.

Kasimamie ukusanyaji wa mapato - Waziri Ummy
Jaji Mkuu Zambia afariki dunia