Diwani wa Kata ya Makonde, Manispaa ya Lindi, Juma Lunda (CUF) amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela baada ya kushindwa kulipa deni la shilingi 785,500.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu ya Wilaya ya Lindi, Lilian Rugalabamo baada ya kujiridhisha kuwa mwanasiasa huyo alishindwa kwa kumalizia kiasi hicho kati ya shilingi milioni 1.5 alizokopa katika Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) miaka saba iliyopita.

Akisoma humu hiyo, Hakimu Rugalabamo alisema kuwa Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa mshitakiwa hakuwa na nia ya kumalizia deni hilo.

Kwa mujibu waelezo yaliwasilishwa mahakamani hapo na SIDO, Makonda alipewa mkopo wa shilingi milioni 1.5 Desemba 11,2007 na kutakiwa kurejesha ndani ya kipindi cha mwaka mmoja lakini hadi Desemba mwaka huu hakuwa amekamilisha deni hilo.

Katika hatua nyingine, Mahakama Kuu ilipitia shauri hilo la Mahakama ya Wilaya ya Lindi na kubaini kuwapo mapungufu katika gharama ya deni kutokana na kutoingizwa kwa gharama za ziada ikiwa ni pamoja na asilimia 5 za kushindwa kulipa deni na shilingi mioni moja kama gharama za kesi na asilimia 22 za intaneti kwa kila mwaka.

Lunda alishindwa kulipa kiasi hicho.

Video: TB Joshua ametutabiria ushindi 2020 - Lowassa, Ajira zamwagwa...
Wastaafu 332 wasotea mafao yao muhimbili