wakala wa utafiti wa vifaa vya ujenzi wa nyumba bora wameshauri kuwa  elimu ya nishati itolewe kwa wadau wa sekta ya ujenzi ili  shughuli  hizo zifanyike kwa kuzingatia   maendeleo endelevu.

Katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mhandisi Benedict Chila amesema katika utafiti unaoendelea kufanyika mikoa mbalimbali nchini wananchi wanateseka na gharama za matumizi ya nishati.

Aidha  amesema kuwa utafiti  huo una lengo la kupunguza kiwango cha nishati kinachotumiwa kwenye nyumba kwa ajili ya kupooza  hewa hivyo kuokoa fedha inayoweza kutumika kufanya mambo mengine ya maendeleo.

hata hivyo Mhandisi Chila amefafanua kuwa utafiti unaoendelea kufanywa na wakala wa utafiti wa vifaa vya ujenzi nchini una dhamira ya kutunza nishati ndogo iliyopo  na kuitumia katika matumizi mengine tofauti na ujenzi .

Aidha Mhandisi Heri ameongeza kwamba kutokana na utafiti walioufanya kwa kipindi kimoja wamegundua kuwa kiwango kikubwa cha miti kinatumika hovyo ili kupambana na hali iliyopo ni elimu zaidi kwa wadau wa ujenzi na wananchi ndiyo zaidi inahitajika.

 

 

 

 

 

 

Hukumu ya Mafisadi itakayotolewa na mahakama ya Mafisadi yawekwa wazi
Young Africans Yaivimbia TFF