Wafugaji wa Fulani nchini Nigeria wameripotiwa kufanya mauaji ya kikatili dhidi ya mwanamke mmoja mkulima, saa chache baada ya mifugo yao kuvamia na kuharibu shamba lake la hekari zaidi ya 200.

Kwa mujibu Sunday Vanguard, baada ya watu hao kumuua Patience Salami mwenye umri wa miaka 67 walimkata viungo vyake vya mwili ikiwa ni pamoja na sehemu za siri, ulimi na moyo kisha wakatokomea navyo.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi, tukio hilo lilitokea wakati ambapo jamii ya wakulima wakaazi wa eneo hilo walikuwa wameenda kwenye sherehe iliyokuwa inafanyika nje ya eneo lao.

Imeelezwa kuwa wafugaji walibadili eneo hilo la wakulima kuwa eneo la malisho siku hiyo na kumshambulia yeyote ambaye alitaka kuwazuia.

Rafiki wa karibu wa marehemu aliyejitambulisha kwa Sunday Vanguard kama Bolanle Raheem mwenye umri wa miaka 65, alisema kuwa alishtushwa na taarifa za mauaji hayo.

Marehemu Patience Salami

“Mmoja kati ya wakulima alinieleza Jumamosi kuwa rafiki yangu aliuawa vibaya. Nilikimbia hadi kwenye eneo la makaazi yake na kushuhudia mwili wa rafiki yangu ulivyoharibiwa,” alisimulia.

Sunday Vanguard imeeleza kuwa polisi wanaendelea kuwatafuta watu hao lakini pia mashamba ya wakulima katika eneo hilo yameharibiwa vibaya.

Wanaume wapigwa marufuku kuwaita wanafunzi wa kike 'baby'
NASA wabadili gia, wapanga kumuweka Raila kwenye kiti cha Kenyatta