Polisi katika kisiwa cha Pemba visiwani Zanzabar nchini Tanzania imepinga vikali kuwa inavunja haki za binadamu kwa kuwatesa na kuwashikilia wapinzani.

Hata hivyo limekiri kuwashikilia baadhi ya wapinzani kwa madai kwamba ni wahalifu.

Hapo jana Muungano wa Upinzani nchini Tanzania ulitoa kauli ya kulaani Polisi huko Pemba kwamba imekuwa ikiwapiga, kuwatesa na kuwafungulia kesi za bandia wafuasi wa upinzani .

Muungano huo tayari umetishia kumpeleka Rais wa Tanzania John Magufuli kwenye mahakama ya kimataifa ya ICC iwapo hataingilia kati mgogoro huo unaoendelea visiwani humo.

Kwa wakati mwingine Mbunge wa jimbo la ubungo ambaye pia ni mwandishi wa habari ameelaani vikali kwa mwandishi wa habari wa habari wa DW kunyang’anywa kitambulisho chake huko zanzibar na kuita ni uonevu usiovumilika.

Ameongeza kwamba kwa sasa waandishi wa habari wamekuwa waoga kutokana na vitisho vya hapa na pale wakiita ni unyanyaswaji wa haki yao ya kiuandishi  Alisema Kubenea wakati akizungumza na DW leo mchana.

Wanamgambo 4 Wauawa na Jeshi la Kenya Lamu
Video: Shirika la kazi Duniani kuandaa tuzo kwa Waajiri