Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Uongozi wa CUF, Julius Mtatiro ameituhumu serikali kuihujumu mahakama kwa kushindwa kuwafikisha viongozi sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama jinsi ambavyo mahakama ilielekeza Machi 27.

Mtatiro amesema kuwa Mahakama baada ya dhamana ya viongozi hao sita wakiongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA , Freeman Mbowe kushindwa kukamilika kutokana na viongozi hao kushindwa kufikishwa mahakamani kutokana na gari la Magereza kuharibika.

Amesema kuwa anafahamu kuwa Serikali ilikuwa na magari pamoja na mafuta ya kumsafirisha usiku wa manane mwanafunzi, Abdul Nondo mpaka  Iringa lakini serikali hiyo hiyo imeshindwa kuwatoa kina Mbowe kutoka Segerea mpaka Kisutu na kushauri kwamba ni muhimu masuala yanapokuwa yamefika mahakamani yaachwe mahakamani.

“Tunatambua mpaka sasa Mwenyekiti mwenza UKAWA, Freeman Mbowe na wenzake bado wapo gerezani, UKAWA inalaumu kwa nguvu zote kitendo cha Serikali na Management ya Magereza kushindwa kuwaleta Washtakiwa Mahakamani, hii ni moja ya hujuma kubwa sana,”amesema Mtatiro

 

 

‘Mikono ya dhahabu’ ya Nelson Mandela yauzwa $10 milioni
Video: Mbowe na wenzake wakwama selo, CAG aomba radhi Watanzania

Comments

comments