Kambi rasmi ya upinzani Bungeni imemuwekea mtego Waziri wa Maliasili na utalii, Profesa Jumanne Maghembe wakihoji uhalali wake wa kuendelea kuiongoza wizara hiyo wakimtwisha mzigo wa upotevu wa mapato za zaidi ya shilingi bilioni 3 kupitia wizara yake.

Akiwasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha katika wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2016/17, Waziri Kivuli wa Wizara hiyo, Ester Matiko alimtaka Rais John Magufuli kujiridhisha endapo Profesa Maghembe anafaa kwakuwa ameshindwa kutekeleza maazimio ya Bunge ya kukusanya tozo kwenye mahoteli ya kitalii yaliyo ndani ya hifadhi za taifa zenye thamani ya shilingi bilioni 3.

Alisema kuwa ingawa maazimio ya Bunge yalipitishwa wakati Profesa Maghembe hakuwa Waziri, anayafahamu maazimio hayo kwani alikuwa Mbunge na kwamba Serikali ni ileile.

“Kitendo cha kutokazia hukumu hiyo na kuisababishia Serikali hasara kubwa namna hii ini uzembe wa hali ya juu wa waziri na watendaji wake. Tunaitaka Mamlaka yake ya uteuzi iridhie kama anafaa kuendelea kuongoza wizara hii ama la, kwasababu amesababisha hasara kubwa,” alisema Matiko.

Akifafanua sakata la tozo hiyo, alisema kuwa wamiliki wa mahoteli yaliyo katika hifadhi hiyo waliipeleka Serikali Mahakamani kupinga tozo hiyo mpya, lakini Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilitoa uamuzi kwa Serikali kuendelea kutoza tozo hiyo. Pia, Mahakama iliitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kutangaza tozo hiyo mpya kwenye gazeti la Serikali ili zianze kutumika mapema.

Mbunge wa CCM ahoji kwanini Mwijage, Mwigulu wasitumbuliwe Jipu
Lowassa azungumzia tuhuma za kukwapua ardhi ya wananchi, Lukuvi aahidi kumnyang’anya