Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kujihakikishia ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu licha ya upinzani mkali wanaoupata kutoka kwa mgombea urais wa Chadema anaengwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa.

CCM imetoa kauli hiyo katika tamko la chama hicho lilisainiwa na mjumbe wa kamati ya ushindi wa chama hicho, January Makamba katika taarifa yake kwa vyombo vya habari ikilaani kitendo wanachodai kilifanywa na wafuasi wa Chadema jijini Tanga, kufanya fujo na kumwaka ‘mkojo’ kwenye ofisi za CCM.

“Tukio la Tanga la Ofisi ya CCM Mkoa wa Tanga kupigwa mawe limewaudhi na kuwakera wana-CCM na wapenda amani wote wa Tanga. Hata hivyo, tumewasihi wana-CCM wasilipize kisasi. Chama chetu kina dhamana ya uongozi wa nchi na ulinzi wa amani ya nchi yetu. Wenzetu dhamana hiyo hawana. Chama chetu kina uhakika wa kushinda na kushika dola, wenzetu wana uhakika wa kushindwa na wamekwishakata tamaa.”

Wiki kadhaa zilizopita, Makamba alitoa taarifa kuwa utafiti unaonesha kuwa CCM itashinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa asilimia 85. Hata hivyo, hakutaja jina la kampuni iliyofanya utafiti huo.

Hata hivyo, Ukawa wamekuwa wakieleza kuwa mwaka huu watashinda kwa asilimia zaidi ya 70 dhidi ya CCM kutokana na utafiti walioufanya wa kitaalam.

 

Van Gaal Akaliwa Kooni Na Mkewe
Kitendo Hiki Kimemsikitisha Lowassa