Abiria katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza wamegoma kupanda vivuko vya MV.Sabasaba na MV Ukara na kutishia kuviponda mawe wakidai kuwa na mashaka  juu ya usalama wa vivuko hivyo.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinadai kwamba mgomo huo umeitishwa na Mwenyekiti wa kijiji cha Bwisya, baada ya kukosa imani na vivuko hivyo ambavyo vinadaiwa kwenda polepole mno, huku kivuko cha MV.Ukara kikisemekana kupakwa lami chini ambayo inawatia wasiwasi.

Hatua hiyo ni kufuatia ajali ya MV Nyerere iliyotokea siku chache zilizopita na kusababisha vifo vya watu zaidi ya mia mbili.

Aidha siku ya jana Balozi wa Kenya, DKT Kazungu amefika Ikulu kutoa pole kwa niaba ya Rais wa Kenya, Uhuru Kenyata ametuma salamu ya rambirambi kufuatia ajali hiyo.

Jeshi la Polisi Sudan Kusini labadilishwa jina
Walimu kupewa kompyuta