Kama kuna maswali mengi ya mtaani ambayo kila mpenzi wa muziki kutoka Tanzani huwa anajiuliza ni juu ya washindi wale wanaotokana na shindano la kutafuta vipaji yaani Bongo Star Search (BSS).

Shindano hili lilianza miaka nane iliyopita na washindi wake kuonekana kushindwa kufurukuta katika kiwanda hiki cha bongo fleva,huku wachache waliofanikiwa kupenya kwenye nafasi zingine wakizidi kupambana mfano Kala Jeremiah, Peter Msechu,kayumba na wengine.

bss.

Hata hivyo kwa kuliona hili Muandaaji wa shindano la BSS Rita Paulsen ‘Madam Rita’ katika Shindano la mwaka jana alitangaza kuwa wana mkataba na Tip Top connection kuwasimamia washindi watano watakaofanya vizuri ili wasije kupotea kama kina Jumanne Iddi na wengineo.

Pamoja na hayo bado ukimya wa wasanii hao watano umezidi kutawala huku Kayumba aliyekua mshindi ndio akionekana zaidi kuliko wenzake ambao wote walikabidhiwa kwenye menijiment moja.

Madam Rita amefunguka juu ya ukimya wa washindi hao watano ambao walikuwa wakionekana na ladha tofauti zenye kuvutia wengi na kudai kwa sasa kazi imebaki kwenyeuongozi wa Tip Top connection kuendeleza vipaji hivyo.

‘sisi tuna mkataba na wakina Babu Tale yaani Tip Top connection wao kuna vitu wanafanya kwa sasa wao kama menejiment. Unajua watu wanahisi amsanii akitoka BSS ana hit siku hiyo hiyo hapana kuna watu wanachukua miaka mtano kumi ndo wanakuja ku hit’ alisema Madam Rita.

Aidha amesema zoezi la menejiment haliwezi kuingiliana na BSS hivyo mapema tu wataanza kutoa tangazo kuhusiana na shindano hilo msimu wa tisa.

 

 

Diva awacharukia Billnas Na Linah, amtumbua Billnas kwenye wimbo wake
Waziri Mkuu Asitisha Vibali Vya Uvunaji Mbao