Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amepiga marufuku baadhi ya watendaji wanaofanya kazi kwa mazoea na kukwamisha harakati za kusukuma maendeleo ya Taifa kwa kasi.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, Desemba 6, 2021 wakati wa kuzindua rasmi kiwanda cha Elsewedy, kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

“Sasa tuachane na mtindo wa kufanya kazi tuliouzoea au ‘business as usual’ kasi yetu iendane na wingi wa wekezaji wanaokuja lakini na viwango vyao pia, kama tulizoea wawekezaji wa $ 8m, $ 9m wanaokuja ni wa madola mengi mengi”.

“Kama mnavyojua tumefanya jituhada kubwa kujenga vyuo vya ufundi, tutakwenda kuweka nguvu na kuangalia ni maeneo gani vijana wetu wafundishwe ili waweze kutumikia viwanda vinavyokuja”.

“Kama nimekubali kubeba mzigo wa kuongoza hii nchi kuna mambo kadhaa yaliyoelekezwa ndani ya Ilani niyatimize, sitayatimiza kwa kukaa ofisini Dodoma au Magogoni lazima nitoke niongee na watu niwashawishi waje kwetu na wakija nihakikishe mambo yamenyooka”.

“Niliahidi kwamba tutajenga chuo kikubwa cha TEHAMA, nataka kuwaambia harakati za awali ziko tayari na muda wowote ujenzi wa chuo hicho utaanza ili vijana wetu wafundishwe mambo ya ICT na waweze kutumika vyema katika uwekezaji unaokuja.

“Unaambiwa ukiwa kiongozi una maswali ya kujibu kwa Mungu, nafanya ninavyoweza ili nikifika huko kesho na keshokutwa nikiulizwa niseme nimefanya hiki kwa usafi, kuliko kwamba ooh nilisema sikusikilizwa, nataka nijisafishie njia yangu”.

Mkurugenzi wa Gereza afungwa miaka 5 jela
Serikali kumfuatilia anayedaiwa kuwa na Omicroni