Imeripotiwa kuwa Uongozi wa klabu ya Young Africans umempa mkono wa kwaheri Kiungo Mshambuliaji wa UD Songo, Jimmy Julio Ukonde, baada ya kushindwa kuonyesha uwezo waliokuwa wanautegemea.

Ukonde alipewa nafasi ya kuwa sehemu ya kikosi cha klabu hiyo kilichoshiriki Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe La Kagame) inayoendelea jijini Dar es salaam.

Mmoja wa viongozi wa Young Africans amefichua siri kuwa, wamegundua kiwango cha Ukonde ni cha kawaida, hivyo hawezi kuisaidia timu yao kwenye michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Barani Africa msimu ujao.

“Ukonde anaondoka leo hatakuwa miongoni mwa nyota tunaotarajia kuwa nao msimu ujao kwa lengo la kuona tunaonyesha ushindani ligi ya ndani na kimataifa, ni mchezaji mzuri lakini hafiti mahitaji ya kocha,” amesema kiongozi huyo.

Ukonde aliwasili Dar es salaam mwishoni mwa mwezi Julai akitokea nchini kwao Msumbiji, alitarajiwa kuonesha kiwango kikubwa kama ilivyo kwa Luis Miquissone wa Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC.

Rais Samia afunguka kesi ya Mbowe, ‘ni ugaidi na uhujumu uchumi’
Aucho afunguka alivyoitosa Simba SC